...MAMA
Eddy aliendelea kukoroma kwa nguvu pale chini na kuzidi kumchanganya
sana mumewe Mr.Alloyce. Mwanaume yule alichanganyikiwa haswa na kujikuta
akiangusha chozi lake kwa uchungu kwani alishindwa kuielewa hali ya
mkewe. Alimuita Mara kadhaa lakini Mama Eddy aliendelea kukoroma tu bila
kujibu neno.
Mr.Alloyce
akazidi kuchanganyikiwa sana bila kuelewa afanye nini na kwa wakati ule
hakukuwa na msaada wowote katika eneo lile. Akachukua simu yake na
kuitafuta namba ya rafiki yake haraka kisha akapiga lakini alipopiga tu
akakutana na maandishi haya " Emergency call only" ndipo akagundua kuwa
sehemu aliyokuwapo haikuwa na mtandao, akazidi kuogopa huku huzuni ya
kupotelewa na mkewe ikimvaa kwa kasi ya ajabu. Kwa muda wote huo hakuna
gari yoyote ilipita eneo lile.
"Na..na..nakufa..nakufa
mume ..wangu.." Ilisikika sauti ya mama Eddy.Sauti ile ya mama Eddy
ilikuwa kama mwiba mchongoma uliopenya katikati ya moyo wa Baba Eddy.
Hakuamini kile alichokisikia kwa mkewe akahisi ilikuwa ndoto tu
isiyokuwa na ukweli wowote.
"Usife
mke wangu.. Usife mpenzi wangu!" Aliropoka Mr.Alloyce lakini tayari
alikuwa amechelewa sana kwani mkewe alikuwa tayari amekata roho.
"Mke
wangu! Mke wangu!" Baba Eddy alijaribu kumuita mkewe lakini tayari
alikuwa ameaga dunia. Simanzi ilimjaa Mr. Alloyce alijkuta Analia kama
mtoto mdogo huku akijigaragaza chini kama mwendawazimu. Alilia kwa
uchungu sana kwani alimpenda mkewe kwa dhati na hakuwa tayari kumpoteza.
Alikuwa ndiye ndugu yake pekee aliyesalia kwani Mr.Alloyce hakuwa na
kaka, Dada wala wazazi.
Wakati
akiwa ameushikilia mwili wa mkewe ghafla akajikuta hajashika chochote
mkononi mwake zaidi ya gauni alilokuwa amevaa mkewe, ndilo pekee
lililombakia mkononi. Akashtuka sana, akajaribu kupepesapepesa macho
huku na kule ili aone mkewe ameenda wapi lakini hakumuona. Mr. Alloyce
akainuka pale chini haraka na kuanza kutimua mbio kwani alishaona hali
si shwari.
Alikimbia
kwa muda mrefu bila kujijua anakimbiaje mpaka pale fahamu zake halisi
zilipomrudia ndipo akasimama kidogo na kupumzika. Alihema kwa nguvu huku
akiwa amejibwaga chini ghafla akasikia mlio mkali ukimjia nyuma yake.
Mr.Alloyce akainuka chini na kuanza kukimbia tena lakini akiwa katika
mbio hizo akapata ufahamu tens akasikiliza tena ule mlio akagundua ni
mlio wa honi ya gari.
Akaamua
kusimama ili aombe msaada. Baada ya muda ya sekunde kadhaa basis la
abiria likitokea Dar es salaam lilikaribia mahali alipo Mr.Alloyce ndipo
alipoanza kupunga mkono ili aombe msaada.
Dereva
wa basi lile alikuwa mwelewa sana, akasimamisha gari na kumsaidia Mr.
Alloyce aliyekuwa akihema sana. Mr.Alloyce alishukuru sana akaingia
ndani ya basi.
"Vipi mbona umeshika gauni hilo mkononi?" Aliuliza kondakta baada ya kumkagua kwa macho Mr.Alloyce
"We acha tu.." Alijibu Mr. Alloyce huku akihema sana.
"Isije ikawa umeua huko halafu sisi tumekusaidia hapa...!" Alisema kondakta.
Mr. Alloyce alikataa kwa kichwa tu kwani hakuweza hata kujibu kutokana na maswahibu yaliyomkuta.
"Haya.. Unashuka wapi?"
"Naenda Ipogoro Iringa!" Alisema Alloyce na kuinamisha kichwa huku akilia.
==> Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
==> Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
TANGAZO LA NDANI===
Facebook Blogger Plugin by SAMCHARDTZ





Chapisha Maoni