Kiongozi
wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na katibu mkuu wa chama cha
wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wamekutana Katika Mkutano Maalum
wa Viongozi wa Kisiasa Ulimwenguni (International Leaders Forum) ambao
umefanyika jana ‘Kwa Saa za Marekani’ Jijini Philadelphia.
Mkutano
huo ulioandaliwa na asasi ya NDI ‘National Democratic Institute’, ni
Sehemu ya matukio maalum kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats
(Democratic National Convention), Mkutano ambao utamthibitisha Bibi
Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais Kupitia Chama Hicho.
Zitto
Kabwe Pamoja Na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim watakuwa Philadelphia mpaka
Siku ya alhamis ambapo mkutano huo unategemewa kumuidhinisha Bi Hillary
Clinton Kuwa Mgombea Urais wa Marekani kupitia Chama Hicho.
TANGAZO LA NDANI===
Facebook Blogger Plugin by SAMCHARDTZ







Chapisha Maoni