
Kampuni hiyo inataka kuchunguza kufahamu ni kwa nini simu hizo zinawaka moto.
Kampuni hiyo ya KOREA KUSINI imesema itasitisha uuzaji wa aina hiyo ya simu.
Kampuni ya SAMSUNG imesema watu walionunua jumla ya simu MILIONI MBILI na LAKI TANO, Septemba wazirejeshe madukani kutokana na malalamiko ya wateja kwamba betri za simu hizo zinalipuka.
Shuhuda wa tukio la kuwaka moto kwa simu hizo mwanamume mmoja wa jimbo la KENTUCKY, MAREKANI amesema aliamka na kukuta chumba kimejaa moshi uliotokana na simu mpya ya hiyo aliyoipata baada ya kurejesha ya zamani.
Shuhuda mwingine ni abiria kwenye ndege moja MAREKANI waliondolewa kwenye ndege kwa dharura baada ya simu ya GALAXY Note 7 kuanza kutoa moshi.
TANGAZO LA NDANI===
Facebook Blogger Plugin by SAMCHARDTZ




Chapisha Maoni