Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.
Loading...
Schweinsteiger arejea kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza Man U
Hatimaye kiungo Bastian Schweinsteiger amerejea kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Man United baada ya kufanya mazoezi mwenyewe au na kikosi cha chini miaka 23 kwa muda wa miezi miwili.
Nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kwa mara ya mwisho aliichezea Man U mwezi Machi wakati Louis van Gaal alipokuwa kocha wa mashetani hao wekundu.
Ligi ya Wanawake kuanza leo Novemba 1, 2016
Ligi ya Taifa ya Wanawake inatarajiwa kuanza leo Jumanne Novemba 1, 2016 katika viwanja sita kuchezwa, ambapo mchezo wa utafanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kati ya wenyeji Baobao dhidi ya Victoria Queens ya Kagera.
Ligi hiyo ya kwanza kufanyika nchini Tanzania, lakini pia kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati imetokea kuvutia wadau kadhaa wakiwamo Azam Tv ambao wamedhamini kwa kuonyesha mubashara (live), michezo 30 itakayofanyika kweny viwanja mbalimbali kwa msimu mzima.
MTV MAMA 2016: Mbivu na mbichi kujulikana Jumamosi hii
Ni tuzo zinazosherehekewa zaidi kuliko zote barani Afrika. Ni tuzo zenye heshima zaidi na maandalizi yake hujumuisha mbwembwe za kila aina.
MTV MAMA 2016, kwa mara nyingine tena inawakutanisha wababe wote wa muziki barani Afrika kwenye jukwaa moja. Mwenyeji mwaka huu, ni jiji la Johannesburg, jijini Afrika Kusini, likipokea kijiti kutoka kwa mji wa Durban uliopata bahati ya kuziandaa kwa miaka miwili mfululizo.

